Proverbs 6

Maonyo Dhidi Ya Upumbavu


1 aMwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,
ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi
kwa ajili ya mwingine,

2 kama umetegwa na ulichosema,
umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,

3 basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,
kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:
Nenda ukajinyenyekeshe kwake;
msihi jirani yako!

4 bUsiruhusu usingizi machoni pako,
usiruhusu kope zako zisinzie.

5 cJiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji,
kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.


6 dEwe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!

7 Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,

8 elakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.


9 fEwe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?

10 gBado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:

11 hhivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyang’anyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.


12 Mtu mbaya sana na mlaghai,
ambaye huzungukazunguka
na maneno ya upotovu,

13 iambaye anakonyeza kwa jicho lake,
anayetoa ishara kwa miguu yake
na kuashiria kwa vidole vyake,

14 jambaye hupanga ubaya
kwa udanganyifu moyoni mwake:
daima huchochea fitina.

15 Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula;
ataangamizwa mara, pasipo msaada.


16 kKuna vitu sita anavyovichukia Bwana,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:

17 lmacho ya kiburi,
ulimi udanganyao,
mikono imwagayo damu isiyo na hatia,

18 mmoyo uwazao mipango miovu,
miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,

19 nshahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,
na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

Onyo Dhidi Ya Uasherati


20 oMwanangu, zishike amri za baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

21 pYafunge katika moyo wako daima,
yakaze kuizunguka shingo yako.

22 qWakati utembeapo, yatakuongoza;
wakati ulalapo, yatakulinda;
wakati uamkapo, yatazungumza nawe.

23 rKwa maana amri hizi ni taa,
mafundisho haya ni mwanga
na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,

24 syakikulinda na mwanamke aliyepotoka,
kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.

25 tMoyo wako usitamani uzuri wake
wala macho yake yasikuteke,

26 ukwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,
hata ukose kipande cha mkate,
naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.

27 Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake
bila nguo zake kuungua?

28 Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka
bila miguu yake kuungua?

29 vNdivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;
hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.


30 Watu hawamdharau mwizi kama akiiba
kukidhi njaa yake wakati ana njaa.

31 wPamoja na hayo, kama akikamatwa,
lazima alipe mara saba,
ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.

32 xLakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.

33 yMapigo na aibu ni fungu lake
na aibu yake haitafutika kamwe;

34 zkwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,
naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.

35 aaHatakubali fidia yoyote;
atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.
Copyright information for SwhKC